08/12/2016
Read this chapter carefully and let's see how's your take on the two brothers, mother and father. A friend told me that this chapter talks about origin of two religions(no proof.... Citation needed) what is your take on it.....
Mwanzo 27:32-42
[32]Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.
[33]Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.
[34]Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.
[35]Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.
[36]Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?
[37]Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu?
[38]Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.
[39]
Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,
Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako,
Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.
[40]Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo;
Na itakuwa utakapoponyoka,
Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.
[41]Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.
Some people have got a very good way of putting this section of the bible.... Let's hear what you think about it.